TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Aliyefutwa na Tottenham kuifunza Villa

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/74815000/jpg/_74815899_74815898.jpg
 Tim Sherwood ameteuliwa kama meneja mpya wa kilabu ya Aston Villa baada ya kuweka sahihi ya kandarasi ya hadi mwaka 2018.
Villa ilimfuta kazi Paul Lambert siku ya jumatano baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi kumi ilizocheza ambapo walifunga bao mbili pekee.
Sherwood mwenye umri wa miaka 46 alichukua mahala pake Andrew Villa Boas kama menaja wa Tottenham mnamo mwezi Disemba mwaka 2013 lakini akafutwa kazi mwishoni mwa msimu uliopita na amekuwa bila kazi wakati wote huo.
''Ni heshima kubwa kusimamia moja ya vilabu vikubwa katika soka ya Uingereza alisema Sherwood.''Siwezi kungojea kuanza na niko tayari kukabiliana na changamoto''.
Sherwood ataiongoiza Villa ambayo imeshindwa kuimarika tangu ilipochukua pointi 10 katika mechi zake nne za kwanza na kufunga mabao 12 kati ya mechi 25
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)