Usitishwaji mapigano unaonekana kudumishwa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wanaongwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukrain.
Eneo
hilo limeripotiwa kutulia tangu makubaliano hayo yalipoanza kutekelezwa
usiku wa manane saa za eneo hilo licha ya kila upande kumlaumu mwingine
kwa kukiuka makubaliano hayo.Msemaji wa jeshi la Ukrain amesema kuwa wametekeleza mashambulizi wakitumia silaha ndogo katika maeneo tisa huku waasi wakiwalaumu wanajeshi wa Ukrain kwa kuwafyatulia risasi karibu na mji wa Debaltseve.
Mapema rais wa Ukrain Petro Poroshenko alisema kuwa ameamrisha wanajeshi wake kuheshimu makubaliano hayo lakini ameonya kuwa Ukrain haitakimya ikiwa makubaliano hayo yatakiukwa.
0 comments:
Post a Comment