Polisi kwenye mji mkuu wa Denmark
Copenhagen wanasema wanaamini kuwa mwanamume waliyemuua kwa kumpiga
risasi ndiye aliyehusika na mashambulizi ya risasi mjini humo.
Polisi
wanasema kuwa walimuua mwanamume huyo alipowafyatulia risasi walipokuwa
wakipiga doria eneo linalokaribiana na mahala ambapo ufyatulianaji
ulifanyika hapo jana.Saa kadhaa zilizokuwa zimepita mwanamume mmoja myahudi alikuwa ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wawili kujeruhiwa katika sinagogi kuu mjini Copenhagen.
Siku ya Jumamosi mwanamume mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye mkahawa mmoja ambapo mjadala kuhusu uhuru wa kujieleza ulikuwa ukifanyika.
Kati ya wale waliokuwa wakihudhuria ni pamoja na mchoraji raia wa sweden ambaye alikuwa amechora vibonzo vya mtume Mohammad akimfananisha na mbwa.
0 comments:
Post a Comment