
Wanaharakati wa haki za binadamu wa muungano wa Ujerumani wa kupiga vita
utumiaji wa watoto kama askari umeitaka Berlin kuzuia silaha kuangukia
mikononi mwa watoto wanaotumiwa katika mizozo ya kivita kama wapiganaji.
Wanaharakati hao wamewasilisha ombi hilo kwa serikali ya Berlin katika
hafla iliyofanyika chini ya anwani "Red Hand Day" kwa lengo la kutiliwa
maanani nafasi ya Ujerumani nchi ya tatu muuzaji wa silaha duniani na
kushadidi wasiwasi juu ya kutumiwa watoto kama askari jeshi katika
mizozo ya kivita. Antje Weber kutoka Muungano huo unaoendesha mapambano
ya kupiga vita utumiaji wa watoto vitani amesema kuwa baadhi ya nyakati,
Ujerumani inaiuzia silaha Saudi Arabia, ambapo Saudia pia huzituma
silaha hizo katika maeneo yenye mizozo kama Syria ambako silaha hizo
hutumika na wakati mwingine hutumbukia mikononi mwa watoto. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, Ujerumani huuza silaha na zana za kijeshi katika
nchi kama Pakistan, India, Misri, Kuwait na Colombia. Ripoti ya hivi
karibuni ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, nchi hizo zina makundi
yanayobeba silaha yanayowatumia watoto kama askari. Ujerumani pia ni
moja ya nchi kubwa zinazounda silaha ndogo ndogo ambazo zinaweza kubebwa
na watoto wadogo kiurahisi.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment