Katibu Mkuu Msaidizi wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) Dkt. Kipyego Cheluget amesema kuwa, eneo hilo la biashara huru litaiunganisha COMESA, Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC. Amesema nchi zote 26 wanachama wa jumuiya hizo tatu za kibiashara zimeeleza nia ya kisiasa ya kuruhusu usafirishaji wa bidhaa na huduma itakapofikia mwishoni mwa mwezi Mei.
Eneo hilo la biashara huru litaanzia Misri hadi Afrika Kusini huku likiwa na idadi ya watu milioni 625 na Pato Ghafi la Ndani (GDP) la takribani dola trilioni moja. Eneo hilo ni takribai nusu ya nchi zote za Umoja wa Afrika na linajumuisha asilimia 58 ya biashara kote Afrika.
Cheluget amesema, nchi zote wanachama zitatakiwa kuridhia makubaliano hayo kabla ya kufunguliwa kwa eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment