Moja ya aina ya story zinazovutia watu
wengi ni pamoja na story ambazo zina matukio ya ajabu ama matukio ambayo
yako tofauti na watu walivyozoea.
Kutoka Zimbabwe kulikuwa na story ambayo ilikaa
kwenye headlines sio za Zimbabwe tu, ila duniani kote; ishu ya Rais wa
nchi hiyo kuanguka wakati akishuka ngazi.
Leo nakupa hii nyingine ya jamaa ambaye amejikuta
akiangukia kwenye mikono ya hakimu wa Mahakama na kuhukumiwa kifungo cha
miaka tisa jela kwa kosa la kula nyama ya chatu !.
Jamaa huyo, Archwell Maramba
alijitetea kwamba mara nyingi amekuwa akila nyama hiyo ili kutibu
maradhi ya uti wa mgongo na imekuwa ikimsaidia kwa kiasi kikubwa sana,
utetezi ambao Mahakama haikuonekana kuujali.
Katika upelelezi wa Polisi walikuta ngozi ya chatu iliyokaushwa pamoja na nyama ndan ya nyumba ya Maramba.
Hukumu hiyo imetokana na jamaa huyo kuonekana
akikiuka sheria ya uhifadhi wa chatu, ambao ni sehemu ya viumbe ambavyo
vinatakiwa kuhifadhiwa na kulindwa.
0 comments:
Post a Comment