TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Matokeo ya leo FEB 8 yaipeleka YANGA kileleni mwa Ligi Kuu T’zania Bara…




Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea hii leo kwa mchezo mmoja uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ukiwakutanisha wenyeji Yanga na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

yangaaaKatika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo ambao walionekana kuutawala kuanzia mwanzo hadi mwisho kitu ambacho kiliwapa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi kwa idadi kubwa ya mabao.
Yanga walifunga mabao yote mawili kupitia kwa kiungo mshambuliaji  Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alifunga mabao mawili baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa Liberia, Kper Sherman.
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Coastal Union kwa bao moja.
Matokeo haya yanawafanya Yanga wapande  kwenye kilele cha ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na idadi ya pointi 25 wakiwazidi mabingwa watetezi Azam FC kwa pointi tatu.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)