
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametembelea mji wa Baga ambao miezi
miwili iliyopita ulishuhudia mauaji ya umati yaliyofanywa na wanamgambo
wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram dhidi ya wakazi wa mji
huo. Katika ziara hiyo ya ghafla rais huyo amezungumza na wakazi na
kuahidi kurejesha amani ya kudumu katika eneo hilo. Rais Goodluck
Jonathan wa Nigeria amewambia waandishi wa habari kwamba, safari yake
katika mji huo ilikuwa na lengo la kuangalia hali ya mambo kwa karibu.
Huku zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu
nchini Nigeria, rais huyo anafanya kila njama kuhakikisha anasalia
madarakani ikiwemo kushadidisha mashambulizi dhidi ya kundi hilo la Boko
Haram ambalo kwa miaka kadhaa limekuwa likitekeleza jinai mbalimbali
dhidi ya raia wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo bila kuchukuliwa
hatua zozote za maana. Aidha hivi karibuni Rais Jonathan aliwahakikishia
wananchi wa taifa hilo hususan wakazi wa majimbo yaliyoko kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo kwamba, muda si mrefu, siku za maombolezo kwa
ajili ya watu wao wanaouwawa kutokana na mashambulio ya kundi la Boko
Haram zitafikia tamati.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment