
Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema kuwa, endapo hatashinda katika
uchaguzi mkuu ujao nchini humo, basi ataondoka bila ya matatizo katika
ulingo wa kisiasa. Al-Bashir aliyasema hayo jana na kuongeza kuwa, kura
za Wasudan ndizo zitakazoamua ima aendelee na siasa au la. Rais huyo wa
Sudan ameyasema hayo katika hali ambayo ana uhakika wa kushinda uchaguzi
huo ujao huku weledi wa mambo wakiyataja matamshi hayo kuwa ya kuwabeza
wapinzani wake. Akizungumza mbele ya wafuasi wake katika eneo la Wad
Madani lililoko katika jimbo la Jazirah alisisitiza kuwa, wananchi wa
Sudan ndio wenye uwezo wa kuamua nani anayestahiki kuongoza taifa hilo.
Rais Omar al-Bashir mwenye umri wa miaka 71 amewakosoa vikali wapinzani
wake waliotangaza tangu mapema kususia uchaguzi ujao. Uchaguzi wa rais
nchini humo umepengwa kufanyika tarehe 13 Aprili mwaka huu. Hii ni
katika hali ambayo vyama vingi vya kisiasa na mashirika kadhaa nchini
Sudan, yametangaza kumuunga mkono rais huyo, suala linalompa uhakika wa
kushinda katika uchaguzi ujao.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment