Serikali ya Algeria na Kenya zimesaini makubaliano ya kushirikiana
katika sekta ya usalishaji mafuta na gesi. Makubaliano hayo yalitiwa
saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Kenya, Amina Mohamed huku
Algeria nayo ikiwakilishwa na Ramtane Lamamra, Waziri wa Mambo ya Nje
wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo yaliyotiwa saini huko
Algiers, mji mkuu wa Algeria, katika kuboresha na kuchochea ustawi wa
viwanda na kiuchumi, nchi hizo zitashirikiana pamoja katika masuala ya
uzalishaji wa mafuta na gesi pia. Makubaliano hayo kati na Nairobi na
Algiers yanajumuisha pia usimamiaji na uwekaji sheria katika sekta ya
mafuta, gesi na nishati, uvumbuzi na uzalishaji vyanzo vya hydrocarbon
nchi kavu na baharini, kupanua viwanda vya petrokemikali, shughuli za
ujenzi wa vinu, kutafuta soko la ndani, usafirishaji na usambazaji wa
mafuta hayo. Hivi karibuni serikali ya Kenya ilitangaza kuwa inatazamiwa
kuanza kuuza mafuta ghafi ya petroli katika soko la kimataifa mwaka
ujao na hivyo kuitangualia nchi jirani ya Uganda ambayo iligundua mafuta
miaka tisa iliyopita.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment