
Chama tawala nchini Senegal kimekosoa utovu wa nidhamu wa rais wa zamani
wa nchi hiyo Abdoulaye Wade dhidi ya Rais Macky Sall. Viongozi wengi wa
serikali mbali na kukosoa matamshi ya Wade dhidi ya Rais Sall,
wamemtaja Wade kuwa ni mtu aliyechanganyikiwa kutokana na uzee. Waziri
Mkuu wa zamani wa Senegal kutoka chama tawala, Aminata Touré amesema
kuwa matamshi ya Abdoulaye Wade yanapingana na mafundisho ya dini ya
Kiislamu. Naye kwa upande wake Youssou Ndour Waziri Mshauri wa serikali
ya Rais Macky Sall amekosoa vikali mwenendo wa rais huyo wa zamani wa
Senegal na kuyataja matamshi yake kuwa hatari. Hivi karibuni Abdoulaye
Wade alimtusi Rais Sall kwamba wazazi wake walikuwa watumwa na wala
nyama za watu, hatua ambayo ameichukua katika kulalamikia kitendo cha
kuzuiliwa mwanawe katika korokoro za serikali kutokana na tuhuma za
ufisadi wa mali za umma. Karim Wade mwana wa Abdoulaye Wade ametupwa
korokoroni tangu mwaka 2013 kwa kosa hilo huku kesi yake ikiwa bado
inaendelea. Shirika la haki za binaadamu nchini Senegal, limeonyeshwa
kusikitishwa na matamshi ya raia huyo wa zamani na kusema kuwa, hakuna
njia nyengine ya kuweza kutetea matamshi hayo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment