Akizungumza mara baada ya kuiongoza timu yake ya taifa, Ivory Coasta, kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika juzi Jumapili usiku, Toure, ambaye alishutumiwa kwa kutojituma kwenye fainali hizo za Afcon, alisema sasa yupo fiti kurejea katika majukumu ya klabu.
YAYA Toure amewaambia wanasoka wenzake wa klabu ya Manchester City kuwa ni lazima wahakikishe wanashinda mechi zilizosalia za Ligi Kuu England kama kweli wanataka kutetea taji.
Akizungumza mara baada ya kuiongoza timu yake ya
taifa, Ivory Coasta, kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika juzi
Jumapili usiku, Toure, ambaye alishutumiwa kwa kutojituma kwenye fainali
hizo za Afcon, alisema sasa yupo fiti kurejea katika majukumu ya klabu.
Hata hivyo, kwa kuwa Man City ipo nyuma ya vinara
Chelsea kwa pointi saba, staa huyo anakiri kwamba haitakuwa kazi rahisi
kupindua mambo.
Toure, nahodha wa Ivory Coast iliyotwaa Afcon juzi
kwa penalti 9-8 mbele ya Ghana, alisema: “Kwa uzoefu wangu nafahamu
soka si mchezo wa mechi moja au mbili, hasa kwenye Ligi Kuu England.
“Tuna mechi 38 na kama tunataka kufanikiwa
(kutetea ubingwa) tunapaswa kushinda michezo hiyo yote. Ninajua ni jambo
gumu, lakini sasa nimemaliza majukumu ya timu ya taifa na ninarudi
kuitetea klabu yangu.”
Mbele ya Ghana juzi, Toure, alifunga penalti yake
katika fainali ambayo pia kipa Boubacar Barry naye alifunga kuhitimisha
ushindi huo wa Ivory Coast.
Kuhusiana na shutuma dhidi yake alisema: “Hata ninapokuwa Manchester kuna watu huwa wananishutumu, kuhusu mambo mengi.
“Wakati fulani unapozungumza ukweli kuhusu soka, watu hawakusikilizi, hasa nyinyi (waandishi wa habari).
Badilikeni. Mara zote mimi ni mtu ninayepigania
mafanikio ya timu, lakini ninajua naweza nisiheshimiwe kwa hilo, ndiyo
soka lilivyo. Lakini kazi yangu ni kujituma uwanjani si kukatishwa tamaa
na watu wanaoketi mbele ya TV zao na kusema wanayojisikia.”
0 comments:
Post a Comment