Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar
nchini Misri, kimeasisi kituo cha elektroniki katika juhudi za
kukabiliana na makundi yenye misimamo ya kufurutu ada na ya kigaidi.
Abas Shuman, mmoja wa viongozi waandamizi wa al-Azhar amesema kuwa,
mbinu za jadi za kuwafikia watu hazitoshi na ndio maana makundi yenye
misimamo mikali yameamua kutumia Intaneti kueneza fikra zao na kwamba,
kwa kuasisiwa kituo hicho cha elektroniki, kutasaidia kukabiliana na
makundi hayo kupitia Intaneti. Shuman amesisitiza kuwa, kituo hicho
kitatumika katika kuwazindua walimwengu kwamba, fikra za kitakfiri,
kufurutu ada na ugaidi ni mambo yasiyo na nafasi kabisa katika Uislamu.
Inaelezwa kuwa, kituo hicho kitatumika pia katika kuzifuatilia, kuzijibu
na hata kuzizuia jumbe na fikra zinazotumwa na wanachama wa kundi la
kitakfiri la Daesh kwa vijana. Hata hivyo Chuo Kikuu cha al Azhar
kimetangaza kuwa, kituo hicho hakitahusika na mashambulizi yoyote ya
kielektroniki dhidi ya vituo vingine vya Intaneti vinavyomilikiwa na
makundi ya kigaidi na kitakfiri.
0 comments:
Post a Comment