Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa, pande hasimu
zina azma ya kupunguza hitilafu zao ili kuwasilisha mapendekezo ya
kimsingi ya kurejesha amani Libya. Mazungumzo hayo yaliyomalizika jana
Jumamosi katika mji wa Skhirat nchini Morocco yalijumuisha serikali
mbili hasimu nchini Libya na alifanyika chini ya upatanishi wa mjumbe
maalumu wa Umoja wa Mataifa Bernardino Leon. Mazungumzo hayo
yanatarajiwa kuendelea wiki ijayo.
Kuwepo serikali mbili na mabunge mawili kwa wakati mmoja
nchini Libya kumesababisha hali ya mkanganyo na mchafukoge kuenea katika
kila pembe ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. Serikali ya kwanza ya
Kongresi ya Kitaifa ina makao yake katika mji mkuu Tripoli na
isiyotambuliwa kimataifa inaungwa mkono na wanagambo wa Fajr Libya.
Serikali ya pili ni ile yenye makao yake mjini Tobruk ambayo
inatambuliwa kimataifa. Hali ya usalama na kisiasa imezidi kuwa mbaya
zaidi nchini Libya baada ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh
kujiingiza ndani ya ardhi ya nchi hiyo na kuishikilia baadhi ya miji
muhimu kama vile Sirte na Darna.
0 comments:
Post a Comment