Afisa mwandamizi wa polisi nchini Tanzania amekanusha tetesi kuwa magaidi wa kundi la Al-Shabab wamekabiliana na vikosi vya usalama katika eneo la Tanga. Kamishna wa Oparesheni katika jeshi la Polisi CP Paul Chagonja amenukuliwa na vyombo vya habari akisema jana kuwa askari wawili wa jeshi la polisi na askari wanne wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ wamejeruhiwa vibaya kwa risasi baada ya kutokea mapigano kati yao na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika mapango ya Amboni mkoani Tanga.
Akitoa taarifa rasmi ya jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo jana
Jumamosi, Chagonja amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Ijumaa
ambapo amesema kuwa si tukio kubwa kama linavyoelezwa na baadhi ya watu
na kwamba waliohusika ni majambazi na siyo magaidi. Amesema kilichotokea
ni oparesheni ya kawaida iliyofanywa na jeshi la polisi kuwasaka watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi waliodaiwa kujificha katika mapango hayo na
ndipo yalipotokea mapigano hayo yaliyoambatana na kurushiana risasi na
kupelekea askari hao kujeruhiwa.
Amesema baada ya hali kuwa tete, jeshi hilo lililazimu kuomba msaada kutoka kwa askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ambao walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kutuliza hali ya taharuki iliyokuwa imetanda katika eneo hilo.

0 comments:
Post a Comment