Wanamgambo wamechukua udhibiti wa majengo kadhaa ya serikali mjini Sirte katika pwani ya Libya.
Ripoti zinasema watu hao waliokuwa na silaha waliingia kwa nguvu katika majengo ya serikali na kuwaamuru wafanyakazi waondoke.
Kati ya majengo yanayodhibitiwa na wanagambo hao ni idara za utawala pamoja na vituo vya radio na televisheni. Maafisa wa serikali ya Libya hawajatoa taarifa yoyote kufuatia tukio hilo. Mji wa Siirte ni makao ya makundi kadhaa ya wanamgambo likiwemo kundi la kitakfiri linalojiita Ansar Sharia. Hayo yanajiri wakati ambao Jeshi la Libya limetangaza kupata mafanikio makubwa dhidi ya makundi ya wabeba silaha katika maeneo ya kusini mwa mji wa Benghazi na kudhibiti maeneo mengi ya mji huo. Kwa mujibu ripoti hiyo, askari wa serikali wakiandamana na vifaru na magari yaliyosheheni silaha za kivita yamekuwa yakilinda doria katika maeneo ya kusini mwa mji huo ambao kwa muda sasa umekuwa ukidhibitiwa na wanamgambo.
0 comments:
Post a Comment