TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Bafetimbi Gomis azirai uwanjani


 Mshambuliaji wa kilabu ya Swansea Bafetimbi Gomis alianguka na kuzirai uwanjani, ikiwa ni kisa cha hivi karibuni cha mchezaji huyo ambaye amekuwa akikabiliwa na tatizo hilo mara kwa mara.
Swansea ilikuwa ikimenyana na kilabu ya Totenham Hospurs wakati wa tukio hilo na kusababisha mchezo kusimamishwa kwa dakika tano ili madaktari kumuhudumia mchezaji huyo.
Mechi hiyo ilikamilika ikiwa Totenham imeibuka kidedea kwa mabao 3-2
Raia huyo wa Ufaransa amekabiliwa na visa kama hivyo ikiwemo visa vitatu alipokuwa akiichezea kilabu ya Lyon mnamo mwaka 2009 na chengine wakati alipokuwa katika kambi ya mazoezi na, wasiwasi uliwazonga wachezaji wenzake katikati ya uwanja alipokuwa akipokea matibabu.


 Huku afisa mmoja wa Swansea akisema kuwa hali ya mchezaji huyo ilikuwa shwari alipokuwa katika chumba cha matibabu katika uwanja wa White Hart Lane baadaye alipelekwa hospitalini ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.
Baadaye mchezaji huyo alituma ujumbe wake katika mtandao wa tweeter akiwashukuru mashabiki kwa kuonyesha umoja wao naye na kuelezea kwamba hali yake ya afya imesababishwa na wasiwasi alionao kuhusu afya ya babaake nchini Ufaransa.



 Aliandika:''Ningependa kuwahakikishia kuhusu afya yangu.
Pengine tukio hilo linaonyesha kwamba afya yangu imezorota ikilinganishwa na nilivyo sasa.
Tatizo hili linasababishwa na uchovu unaosababishwa na wasiwasi nilionao kuhusu afya ya babaangu ambapo mimi hulazimika kusafiri kwa mda mrefu kwenda na kutoka Ufaransa kila mara''.



Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)