Patrick Spirlet, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi amesema hayo akiwa mjini Bujumbura na kusisitiza kwamba, kusimama Rais Pierre Nkurunziza kwa ajili ya kugombea katika uchaguzi ujao wa Rais ni hatari na kunaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa na machafuko.
Mwakilishi huyo wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi ameashiria malalamiko ya wananchi dhidi ya hatua ya kugombea tena Nkurunziza katika uchaguzi ujao na kusema kuwa, kwa mtazamo wa Umoja wa Ulaya kugombea Nkurunziza kwa mara ya tatu kunaweza kuitumbukiza Burundi katika mivutano na machafuko na hatimaye nchi hiyo kukabiliwa na hatari.
Hatua ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutangaza nia yake ya kuwania tena kiti cha urais, imekabiliwa na malalamiko mengi nchini Burundi zikiwemo asasi za kiraia, wapinzani wa serikali na kanisa katoliki. Uchaguzi wa Rais nchini Burundi umepangwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment