TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Makuei: Mazungumzo ya S/Kusini yana vizingiti vingi

Makuei: Mazungumzo ya S/Kusini yana vizingiti vingiSerikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa, mazungumzo yake na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar yanakabiliwa na vizingiti vigumu. Msemaji wa timu ya serikali katika mazungumzo na waasi Michael Makuei amebainisha kuwa, waasi wa nchi hiyo wamekuja na mambo mapya jambo ambalo limeufanya mwenendo wa mazungumzo hayo kukabiliwa na kikwazo. Afisa huyo mwandamizi katika mazungumzo na waasi amesisitiza kuwa, waasi hao hawako makini katika mazungumzo na wanataka kuvunjwa Bunge na asasi nyingine hususan Kamisheni ya Taifa ya Uchaguzi, Kamisheni ya Taifa ya Kutazama Upya Katiba, vyombo vya mahakama na kubadilishwa wajumbe na viongozi wote wa taasisi hizo.
Wakati huo huo Pout Kang, msemaji wa waasi wa Sudan Kusini ametangaza kuwa, hawajafikia makubaliano yoyote yale na serikali ya Juba. Hayo yanajiri katika hali ambayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni liliunga mkono azimio la kuziwekea vikwazo pande mbili hasimu za Sudan Kusini, endapo hazitafikia makubaliano katika muda ulioainishwa ambao ulimalizika jana.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)