Wagonjwa wanaotibiwa na dawa za
viuavijasumu ama antibiotics mara kwa mara huenda wakakabiliwa na hatari
ya kupatwa na aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari ,watafiti wamegundua.
Utafiti uliochapishwa na Jarida la utafiti wa damu ulifuatilia dawa zinazopewa mamilioni ya wagonjwa nchini Uingereza.Waanzilishi wa utafiti huo wanasema kuwa matokeo ya utafiti huo hayamaanishi kwamba dawa hizo husababisha kisukari ,na badala yake maambukizi huenda ni ishara za mapema kwamba mtu anakabiliwa na kisukari.
Wanasema kuwa kazi ya ziada inahitajika ili kuelewa uhusiano huo.
''Ni utafiti mkubwa na wenye usaidizi unaohusisha kisukari na utumiaji wa dawa za viuavijasumu miongoni mwa wakaazi wa Uingereza,lakini kufikia sasa hatujui ni kipi kilichokuja mwanzo,ni kuku ama ni mayai yake'',professa Jodi Lindsay wa chuo cha St Georges mjini London alisema.
Utafiti huo uliangazia idadi ya dawa hizo zilipewa wagonjwa 208,000 wa kisukari cha aina ya kwanza na ya pili mwaka mmoja kabla ya kupatikana na ugonjwa huo ikilinganishwa na watu 816,000 wasio na ugonjwa huo walio na umri sawa na jinsia sawa.
0 comments:
Post a Comment