
Muungano wa vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
umetangaza kuwa hautashiriki kwenye uchaguzi wa mabaraza ya mikoa. Vyama
67 vya upinzani nchini Kongo vimetangaza kuwa havitawaarifisha wagombea
wao katika uchaguzi huo, iwapo tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo
haitatangaza orodha ya uchaguzi wa mabaraza ya mikoa kabla ya kufanyika
uchaguzi. Vyama hivyo 67 vya upinzani huko Kongo ambavyo vitatu kati
yake vina wabunge katika bunge la taifa la nchi hiyo, vimetaka kukutana
na kufanya mazungumzo na maafisa wa tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo
ili kujadili suala hilo. Uchaguzi wa mabaraza ya mikoa huko Kongo DR
umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, huku vyama vikiwa na fursa
ya kuwaarifisha wagombea wao hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu. L'abbe
Malu Malu Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka huu wa 2015 na 2016, chaguzi
saba zitafanyika nchini, ambapo uchaguzi wa kwanza utakuwa ni wa
mabaraza ya mikoa na wa mwisho utakuwa wa Rais ambao utafanyika mwishoni
mwa mwaka kesho wa 2016.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment