
Habari kutokna nchini Misri zinaonesha kuongezeka mwenendo wa hukumu
kali na za kidhulma dhidi ya wapinzani na matukio ya nchi hiyo
yanaonesha kuwa, vyombo vya mahakama vya nchi hiyo kivitendo vimegeuzwa
na watawala wa Misri na kuwa wenzo wao wa kuwakandamiza wapinzani lengo
likiwa ni kunyamazisha sauti yoyote ile ya malalamiko. Kuhusiana na
hilo, Rais aliyepinduliwa na jeshi Muhammad Mursi amehukumiwa kifungo
cha miaka 20 jela. Mahakama ya Jinai ya Cairo Jumanne ya jana ilimhukumu
kifungo cha miaka 20 jela Muhammad Mursi kwa tuhuma za kuchochea
machafuko, mauaji na kuwatesa waandamanaji. Hili ni faili la kwanza la
kesi miongoni mwa mafaili matano ya kesi zinazomkabili Mursi. Rais huyo
wa zamani wa Misri anaweza kukata rufaa kulalamikia hukumu hiyo ya
mahakama ya jinai. Hii ni hukumu ya kwanza kutolewa dhidi ya Mursi tangu
alipoondolewa madarakani na jeshi tarehe 3 Julai mwaka 2013; na
imepangwa kuwa tarehe 16 ya mwezi ujao wa Mei, Mursi atasomewa mashtaka
ya mafaili mengine mawili ya kesi zinazomkabili. Ikumbukwe kuwa,
Muhammad Mursi alikuwa Rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kupitia
uchaguzi huru na aliondolewa madarakani mwaka mmoja tu baada ya kuwa
madarakani. Hadi sasa mamia ya wafuasi wa Mursi wamehukumiwa adhabu ya
kifo ambapo Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hukumu kama hizo ni za
aina yake na hazijawahi kushuhudiwa. Wakati Muhammad Mursi anasota jela
na akiwa anakabiliwa na hukumu kali. Hivi karibuni Hosni Mubarak
dikteta wa zamani wa Misri na wanawe walifutiwa tuhuma na mashtaka yote
yaliyokuwa yakiwakabili. Hatua ya Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri ya
kumfutia mashtaka Hosni Mubarak na kumhukumu Mursi inalenga kutokomeza
mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo,
ukandamizaji na mipango ya kutaka kuwafuta katika ulingo wa siasa za
Misri wanachama wa Ikhwanul Muslimiin nayo imo katika sera za serikali
na vyombo vya mahakama vya nchi hiyo. Katika kipindi hiki wanaharakati
elfu 22 wa kisiasa wametiwa mbaroni na jeshi na vyombo vya usalama vya
Misri na takribani mia mbili kati yao wamehukumiwa adhabu ya kifo.
Kushadidi vitendo vya utumiaji mabavu na kutolewa hukumu kali na za
kidhulma nchini Misri dhidi ya wapinzani wa kisiasa kumezitia wasiwasi
mkubwa fikra za waliowengi ulimwenguni pamoja na asasi za kutetea haki
za binadamu. Licha ya yote hayo wafuasi wa Muhammad Mursi wangali
wanamtambua jenerali wa kijeshi Abdul Fattah al-Sisi kwamba, ndiye
aliyeongoza wa mapinduzi ya kijeshi na ambaye alipuuza matokeo ya
uchaguzi wa Rais wa mwaka 2012 na kumuondoa madarakani Muhammad Mursi
Rais halali aliyekuwa ameibuka na ushindi kupitia uchaguzi halali na wa
wazi. Wanaharakati wa kisiasa nchini Misri wanasisitiza kwamba, uchaguzi
uliokuja kufanyika baadaye na kupelekea jenerali al-Sisi kuibuka na
ushindi, ulikuwa wa kimaonyesho na kiini macho cha kuhalalisha mapinduzi
ya kijeshi dhidi ya Mursi. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa,
kuendelea malalamiko ya wananchi wa Misri ambako kunahesabiwa kuwa ni
mtihani wa kupima azma na irada ya fikra za waliowengi ulimwenguni
mkabala na wanajeshi wa nchi hiyo kunaweka wazi suala hili kwamba,
viongozi wa sasa wa Misri wanatoa hukumu kali na za kidhulma ili kuleta
wasiwasi na woga na wakati huo huo kujaribu kuhalalisha suala la
kumuondoa madarakani Muhammad Mursi.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment