Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, linaendelea kupata ushindi katika
vita vyake dhidi ya kundi la Boko Haram na hadi sasa limefanikiwa kuteka
kiwango kikubwa cha silaha za kundi hilo ambalo limekimbia katika mji
wa Baga baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi. Msemaji mmoja wa jeshi la
Nigeria amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, jeshi la Nigeria
hivi sasa linaendesha operesheni ya kuuzingira na kuwasaka wanamgambo wa
Boko Haram katika mji wa Baga na limefanikiwa kukamata silaha nyingi
zilizoachwa nyuma na wanamgambo hao ambao wanaendelea kukimbia huku na
huko. Mji wa Baga ni moja ya maeneo muhimu ya uvuvi katika fukwe za Ziwa
Chad, kaskazini mwa jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mji huo ulikombolewa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram juzi
Jumamosi. Kundi la Boko Haram ambalo lina welewa finyu kuhusu mafundisho
ya dini tukufu ya Kiislamu lilianzisha mashambulio ya kigaidi katika
maeneo mbalimbali ya Nigeria mwaka 2009, na limetangaza kuhusika katika
utegaji mabomu, ufanyatuaji risasi, mashambulizi ya kutisha na jinai
mbalimbali ndani ya Nigeria na katika nchi jirani. Zaidi ya watu 13 elfu
wamesharipotiwa kuuawa hadi hivi sasa na milioni moja na nusu wengine
kuwa wakimbizi kutokana na mashambulio hayo ya Boko Haram.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment