Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema kuwa ni uhaini kwa yoyote
kufanya njama ya kutaka kuasisi serikali ya muda nchini Nigeria. Rais wa
Nigeria ameyasema hayo Jumapili hii huko Abuja mji mkuu wa nchi hiyo
katika mkutano na Maaskofu wa Katoliki wa Nigeria. Rais Goodluck wa
Jonathan ameyasema hayo siku kadhaa baada ya Rais wa zamani wa nchi hiyo
Olusegun Obasanjo kudai kuwa Rais Jonathan anapanga kufanya udanganyifu
katika uchaguzi au kusababisha mgogoro ili asalie madarakani. Hata
hivyo Rais Jonathan amesema kuwa ana imani kuwa Nigeria itaendelea kuwa
tulivu na kusisitiza kwamba uongozi wa muda nchini humo pia ni kinyume
cha katiba. Reuben Abati, Msemaji wa Rais wa Nigeria hivi karibuni
alimtuhumu Rais wa zamani wa nchi hiyo Olusegun Obasanjo kuwa anafanya
njama na wengine ili kuchochea mgogoro na kuasisi serikali ya muda
nchini Nigeria.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment