Taarifa iliyotolewa na maaskofu hao pia imelaani vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wanamgambo hao kwa kutumia jina la Ukristo. Imeongeza kuwa, kabla ya Anti-Balaka kutekeleza pendekezo la Umoja wa Mataifa la kuwalinda raia, wanatakiwa kuweka chini silaha zao kwa hiari na kushiriki katika mchakato wa serikali katika kurejesha usalama na utulivu nchini.
Kwa mujibu wa azimio nambari 2149 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuanzia mwezi Julai mwaka huu, kutaanza operesheni kali ya kuyapokonya silaha kwa nguvu makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mapigano baina ya waasi wa zamani wa Seleka na kundi la Kikristo la Anti-Balaka yalianza mwishoni wa mwaka 2012, na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu na wengine kuwa wakimbizi wengi wao wakiwa Waislamu.
0 comments:
Post a Comment