Siku kama ya leo miaka mitano iliyopita Abdulmalik Rigi kiongozi wa kundi la kigaidi la Jundullah lenye makao yake huko Pakistan, alitiwa mbaroni katika oparesheni tata ya kiintelijinsia iliyofanywa na maajenti wa Wizara ya Usalama wa Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Baada ya kufanya mashambulizi mengi ya kigaidi, gaidi huyo katili alikuwa safarini kuelekea nchini Kyrgyzstan akitokea Dubai, Imarati, kwenda kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani. Hata hivyo wana usalama wa Iran waliokuwa wakifuatilia kwwa karibu nyendo zake waliweza kuitambua ndege iliyokuwa imembeba gaidi huyo na kuisubiri iingie katika anga ya Iran na hivyo kuilazimisha kutua katika uwanja wa ndege wa Bandar Abbas wa kusini mwa Iran na baadae wakamtia mbaroni kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la Jundullah. Rubani wa ndege hiyo alifanya jitihada kubwa za kutoroka na kutoka nje ya anga ya Iran, lakini alizidiwa nguvu na maafisa usalama wa Iran, na kulazimishwa kuishusha chini ndege hiyo kabla haijaingia kwenye anga ya Imarati. Abdulmalik Rigi alifanya jinai nyingi ikiwa ni pamoja na kutega na kuripua mabomu katika maeneo ya umma nchini Iran, kuwauwa kwa umati raia pamoja na kuwateka nyara. Rigi hakuwa na huruma hata kwa watu wake wa karibu. Abdulmalik Rigi alikiri kwamba alikuwa anapata misaada ya kila namna ikiwemo ya kifedha na kisilaha kutoka kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kama njia ya kuliwezesha kundi lake lifanye mauaji ya watu ndani ya Iran hususan katika maeneo ya kusini mashariki mwa Iran na kusababisha mizozo ya kimadhehebu katika maeneo hayo. Gaidi huyo alinyongwa tarehe 30 Khordad mwaka 1389 Hijria Shamsia sawa na tarehe 20 Juni, 2010 Milaadia yaani miezi minne baada ya kutiwa mbaroni. Kukiri huko kwa Rigi kunaonyesha wazi madai ya uwongo ya serikali ya Marekani ya eti inapambana na ugaidi.
*******
Siku kama ya leo miaka 129 iliyopita, Charles Martin Hall, mvumbuzi
na mwanakemia wa Marekani alifanikiwa kuvumbua njia mpya ya upatikanaji
wa aluminiamu. Aluminiamu ni chuma cheupe na chepesi kinachoweza
kukunjwa kwa urahisi. Aluminiamu hiyo ambayo ni nyepesi kuliko chuma,
leo hii imekuwa na matumizi mengi katika shughuli za viwanda na
kadhalika.
*******
Siku kama ya leo miaka 216 iliyopita, Napoleon Bonaparte mfalme wa
Ufaransa, alianza kuishambulia Sham, ambayo wakati huo ilikuwa ikiundwa
na nchi za Syria, Jordan, Lebanon na Palestina. Mashambulio ya Bonaparte
dhidi ya Misri yalifanyika kwa lengo la kutoa pigo kwa Uingereza
iliyokuwa mkoloni wa Misri. Sababu ya mashambulio ya Napoleon Bonaparte
dhidi ya Sham iliyokuwa sehemu ya ardhi ya utawala wa Othmania, ilikuwa
ni hatua ya mfalme wa utawala wa Othmania ya kutangaza vita dhidi ya
Ufaransa. Katika mashambulio hayo, na licha ya kwamba awali Bonaparte
alipata ushindi, lakini baadaye alilazimika kuacha vita na kurejea kwao
kutokana na uungaji mkono wa Uingereza na Urusi kwa utawala wa Othmania
bila kusahau kuharibika hali ya mambo ndani ya Ufaransa.
*******
Na siku kama ya leo miaka 65 iliyopita, alifariki dunia Haidar Qali
Khan Afghani, maarufu kwa jina la Sardor Kabili, msomi mkubwa wa
Kiislamu. Alikuwa mtaalamu mkubwa wa elimu kama vile hisabati, nyota,
historia, jiografia, falsafa, mantiki na fasihi ya lugha ya Kiarabu.
Sardor Kabuli alikuwa na mapenzi makubwa na watu wa kizazi cha Bwana
Mtume Muhammad (saw) na aliandika kitabu kilichoelezea fadhila za Imam
Ali (as). Msomi huyo ameacha vitabu mbalimbali moja wapo kikiwa kitabu
cha ‘Sharhu Duaye Nudbeh’ na ‘Munadharaat’.
0 comments:
Post a Comment