
Waziri wa Usalama wa Marekani
anasema analitia maanani sana tishio la kundi la Waislamu wa Somalia, Al
Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya maduka huko Marekani, Canada na
Uingereza.
Katika mahojiano kwenye televisheni, Jeh Johnson
alisema pametokea mabadiliko katika vitisho vya makundi ya wapiganaji
Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa washabiki wao katika nchi maalumu
kufanya mashambulio.
Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali
Mwaka
wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la
Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment