Ofisi ya haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, imelaani vikali
vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyofanywa na mashabiki wa kandanda
kutoka klabu ya Uingereza ya Chelsea, wakati klabu hiyo ikijiandaa
kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mjini Paris Jumanne
iliyopita. Mashabiki hao wa Chelsea walinaswa kwenye kamera wakiimba
nyimbo za kujigamba kwa ubaguzi wao wa rangi, huku wakimzuia raia mmoja
wa Ufaransa mwenye asili ya Afrika kupanda kwenye treni kwa kumsukuma
nje. Ofisi ya Haki za Binadamu imesema katika miaka ya hivi karibuni,
imekuwa ikifanya mashauriano na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA na
Shirika la Soka Ulaya, UEFA kuhusu kutafuta njia za kuendeleza juhudi za
kutokomeza ubaguzi wa rangi katika mchezo wa kandanda baada ya matukio
mengi ya vitendo vya kibaguzi, hususan ndani ya viwanja vya mpira.
Rupert Colville ni msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu amesema: "Hili
siyo tukio moja tu, vitendo kama hivi vya kikatili na ubaguzi wa rangi
hutokea kila siku barani Ulaya lakini haviibui hasira kiasi hicho kwa
kuwa havinaswi kwenye kamera." Amesema vitendo vya stesheni ya treni ya
Richelieu-Drouot mjini Paris vimeonyesha kuwa bado kuna kazi nyingi ya
kufanya kabla ya kutokomeza ubaguzi wa rangi katika soka na katika jamii
kwa ujumla.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment