
Mmoja wa wanamgambo wa Tunisia aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba
ambaye pia ni kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Daesh
ameuawa katika mapigano nchini Libya. Mohammed Ali Aroui, msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia amesema kuwa kifo cha kamanda huyo
wa Daesh kwa jina la Ahmed al Rouissi kimethibitishwa kupitia njia za
kitaalamu ambazo zilitumiwa kwa kushirikiana na maafisa wa Libya.
Mwanachama huyo wa kundi la Daesh aliuliwa kwenye mapigano katika mji wa
pwani wa Sirte kati ya kundi hilo na wapiganaji watiifu kwa kundi
linaloudhibiti mji mkuu Tripoli lenye makao yake katika mji wa Misrata.
Kamanda wa ngazi ya juu wa Daesh aliyeuliwa huko Libya anaaminika kuwa
ndiye aliyekuwa akipanga mashambulizi mengi ya kigaidi huko nchini
Tunisia yaliyokuwa yakitekelezwa na kundi la Kisalafi na lile la Ansarul
Sharia, yakiwemo mauaji ya wanasiasa wa nchi hiyo Chokri Belaid na
Mohamed Brahmi.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment