
Nigeria imesema kuwa imeanzisha shambulio la mwisho dhidi ya wanamgambo
wa kitakfiri wa Boko Haram kabla ya kufanyika uchaguzi wa Rais tarehe 28
mwezi huu. Mike Omeri, msemaji wa serikali ya Nigeria amesema kuwa
vikosi vya nchi hiyo vinafanya bidii kubwa na kwamba wanaelekea katika
mashambulio ya mwisho dhidi ya Boko Haram, kwa sababu tayari
wameshaanzisha oparesheni kuanzia huko Bama katika jimbo la Borno.
Amesema kuwa mji wa Bama ulikombolewa juzi na kwamba maeneo ambayo bado
hayajakombolewa ni Abadam, Gwoza na Askira. Msemaji wa serikali ya
Nigeria ameongeza kuwa mafanikio makubwa ya kistratejia yamepatikana
dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram katika wiki za hivi karibuni. Mji wa
Bama ulikuwa ukishikiliwa na Boko Haram tangu mapema mwezi Septemba
mwaka jana wakati ulipodhibitiwa na kundi hilo pamoja na miji na vijiji
kadhaa katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe katika mpaka wa nchi
hiyo na Chad, Cameroon na Niger. Jeshi la Nigeria huku likisaidiwa na
Chad, Niger na Cameroon limekuwa likifanya oparesheni tafauti katika
miezi ya hivi karibuni ili kurejesha utulivu katika maeneo ya kaskazini
mashariki mwa nchi kabla ya kufanyika uchaguzi wa Rais.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment