Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Novemba mwaka 2013, yaani wakati yaliposainiwa makubaliano ya muda ya nyuklia mjini Geneva kati ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1, utekelezaji wa sheria hiyo ya hali ya hatari kitaifa ulirefushwa pia; na wakati Iran ilipolalamikia hatua hiyo Ikulu ya Marekani ilitoa kauli tu ya kudai kwamba ‘urefushwaji huo ni utaratibu wa kawaida katika siasa za Marekani’ ambao lazima ufanyike kila mwaka ili kuepusha kupita tarehe ya kusainiwa kwake. Lakini ukweli ni kwamba kurefushwa kwa hali hiyo kuna ujumbe uliojificha ambao ni kuonyesha kwamba serikali ya Marekani ingali inaendelea kufuata mitazamo yake ya kisiasa ya huko nyuma. Na hayo yanafanyika ilhali kuhitimishwa vikwazo kumetajwa kuwa moja ya vipimo muhimu vya kuzingatiwa katika makubaliano kamili na rasmi ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1; na kwa hivyo uamuzi huo unaweza kutafsiriwa kuwa ni ishara ya kuendelezwa siasa zinazotekelezwa waziwazi na mrengo maalumu ndani ya Kongresi ya Marekani. Nukta nyengine ni kwamba kurefushwa bila sababu hali ya hatari kuhusiana na Iran ni uendelezaji pia wa sera ya “kueneza hofu juu ya Iran” ambayo imetumiwa kwa miaka kadhaa kama kisingizio hewa cha kuandaa mazingira ya kupinga shughuli za amani za nyuklia za Iran. Kwa upande mwengine hatua hiyo inadhihirisha pia njama za wazi na za kificho za Marekani za kutaka kuitia doa nafasi kuu ya Iran katika kukabiliana na machafuko katika eneo hili la Mashariki ya Kati hususan katika mapambano dhidi ya ugaidi. Hali ya kuwa Jamii ya Kimataifa na nchi za eneo zinakiri kwamba Iran imekuwa na nafasi kuu katika kupambana na ugaidi katika eneo hili. Katika suala la kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya pia yanayotishia usalama wa eneo na ulimwengu kwa jumla, mchango chanya wa Iran umekuwa ukipongezwa kila mara na Umoja wa Mataifa pamoja na nchi za Ulaya. Kwa hivyo inabidi tujiulize, ni kitisho gani inachotoa Iran kwa Marekani cha kumfanya Rais wa nchi hiyo arefushe kila mwaka sheria ya hali hatari kitaifa kuhusiana na Iran? Hali ya kuwa ni Marekani ambayo kwa muda wa zaidi ya miongo mitatu mtawalia imekuwa ikitishia usalama wa Iran kutokana na sera zake za vitisho na za kuunga mkono mtandao wa al Qaeda na makundi mengine ya kigaidi. Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden alishawahi kukiri kwamba baadhi ya nchi za eneo ikiwemo Saudi Arabia, Uturuki na Qatar, ambazo ni waitifaki wa Washington zimetumia mamia ya mamilioni ya dola na kutoa maelfu ya tani za silaha kuyasaidia makundi ya kigaidi yenye mfungamano na al Qaeda yakiwemo ya Jabhatun Nusra na Daesh. Hata hivyo Marekani haizichukulii hatua kama hizo kuwa ni tishio kwa usalama wake wa taifa kwa sababu yenyewe ni sehemu ya wafadhili wa magaidi hao. Katika hali kama hii ni jambo la kulitafakari mno dai kwamba Iran ingali ni tishio lisilo la kawaida kwa usalama wa taifa wa Marekani. Kurefushwa kwa hali hiyo kila mwaka, badala ya kufanywa kutokana na tathmini halisi za kiusalama kunachochewa na utashi wa kisiasa tu. Hata hivyo Marekani haitoweza kuyapuuza milele mabadiliko ya kisiasa na ya jiopolitiki katika eneo hili na kudhani kwamba kwa kurefusha sheria hiyo itaweza daima kuendelea kuitupia Iran mpira wa lawama…/
Marekani na urefushaji wa sheria ya ‘tishio lisilo la kawaida’ la Iran

0 comments:
Post a Comment