Waziri Katika Ofisi ya Rais nchini Niger Mohammad Bazoum amesema nchi yake imedhibiti hali ya mambo na kwamba magaidi wa Boko Haram hawawezi tena kuchukua udhibiti wa mji wowote. Siku ya Jumatano msemaji wa pilisi nchini Niger Kepteni Adili Toro alisema tokea Februari mwaka 2015, nchi yake imeangamiza magaidi wapatao 500 wa Boko Haram kutoka nchi jirani ya Nigeria. Mnamo Machi 8 Chad na Niger zilianzisha oparesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya magaidi wa Boko Haram kama sehemu ya jitihada za kieneo za kuangamiza kundi hilo la kitakfiri lenye makao yake kaskazini mwa Nigeria.
Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Zaidi ya watu elfu 13 wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
0 comments:
Post a Comment