Jana Jumamosi, Baraza la Nidhamu katika Mhakama ya Rufaa Cairo liilitangaza uamuzi wa kuwalazimisha majaji 31 kustaafu baada ya kubainika kuwa walitai saini taarifa ya kumuunga mkono Morsi katika maandamano ya 2013. Baraza hilo limesema majaji hao wamekiuka kanuni cha mahakama cha Misri kwa kujihusisha katika harakati za kisiasa. Hii ni katika hali ambayo majaji waliounga mkono mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013 hawajachukuliwa hatua yoyote pamoja na kuwa walibainisha maoni yao wazi wazi. Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yameikisoa vikali serikali ya Rais Abdel Fattal el-Sisi kwa kutekeleza sera za ukandamizaji wa wapinzani nchini humo. Imearifiwa kuwa watu 1,400 wameuawa na wengine 22, 000 kutiwa mbaroni na kuhukumiwa kifo kwa umati katika kampeni ya serikli dhidi ya wafuasi wa Mori, rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia huru nchini Misri. Morsi alitimuliwa madarakano Julai 2013 katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na el Sisi ambaye wakati huo alikuwa kamanda wa jeshi.
Misri yawatimua majaji waliomuunga mkono Morsi

0 comments:
Post a Comment