Rais Barack Obama wa Marekani amerefusha vikwazo dhidi ya Rais Robert
Mugabe wa Zimbabwe na watu wake wa karibu, huku serikali ya Uingereza
ikimtuma Zimbabwe Waziri wake wa Maendeleo ya Kimataifa kwa ajili ya
mazungumzo na utawala wa Harare. Chama tawala cha Zimbabwe Zanu-pf
kimelaani hatua hiyo ya Rais wa Marekani ya kurefusha muda wa vikwazo
dhidi ya Rais Mugabe na watu wake wa karibu. Obama amesema kuwa tishio
lililotokana na vitendo na sera za baadhi ya wanachama wa serikali ya
Zimbabwe na watu wengine za kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia nchini
humo bado lipo pale pale. Amesema ni kutokana na sababu hiyo ndio maana
ameona kuna umuhimu wa kuendeleza kwa nguvu vikwazo kwa Rais Mugabe na
watu wake wa karibu ili wachukue hatua kuhusu suala hilo. Hata hivyo
katika upande wa hatua chanya kwa Harare, serikali ya Uingereza
imethibitisha kuwa, Mark Lowcock Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa
nchi hiyo wiki hii ataelekea Zimbabwe kwa ajili ya mazungumzo na Patrick
Chinamasa Waziri wa Fedha na maafisa wengine wa nchi hiyo. Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza amesema kuwa, nchi yake itaendelea
kuwasaidia watu maskini wa Zimbabwe na kufanya kila inaloweza ili
kuimarisha demokrasia, uthabiti na ustawi katika nchi hiyo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment