Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeitaja ripoti ya Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International dhidi ya muqawama wa Palestina huko Ghaza kuwa inalenga kuhalalisha jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika ripoti yake kuhusu mashambulio ya kikatili ya siku 50 ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza, ya mwezi Julai 2014, shirika la Amnesty International limedai kuwa, mashambulizi ya makombora ya makundi ya Palestina katika maeneo ya Israel yaliyoua walowezi kadhaa wa Kizayuni ni jinai ya kivita. Hii ni katika hali ambayo, zaidi ya Wapelestina 2,300 ikiwemo idadi kubwa ya wanawake na watoto wadogo waliuawa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya siku 50 ya jeshi katili ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, na zaidi ya Wapalestina 11 elfu walijeruhiwa. Hata hivyo shirika la Amnesty International limetoa ripoti ya kuunga mkono jinai hizo za Wazayuni. Bw. Ismail Ridhwan, mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya HAMAS alisema jana kuwa, ripoti hiyo ya Amnesty International ni ya kidhulma na si ya kiuadilifu hata kidogo. Alisisitiza kuwa, katika ripoti yake hiyo, shirika hilo limewaweka kwenye handaki na daraja moja nduli katili na muhanga aliyefanyiwa unduli na ukatili huo. Amesema, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, muqawama ni haki ya kisheria kwa Wapalestina wanaolinda ardhi yao iliyotekwa na kukaliwa kwa mabavu na walowezi wa Kizayuni. Wakati huo huo Salah al Bardawil, kiongozi mwingine mwandamizi wa HAMAS ameituhumu Amnesty International kuwa nayo imetenda jinai dhidi ya Palestina kwa ripoti yake hiyo ya kidhulma. Katika upande mwingine, Issa Amro, mchambuzi wa masuala ya kisiasa ameiambia televisheni ya Press TV kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni mvunjaji mkubwa wa haki za binadamu na kuongeza kwamba, kuwaua kwa umati zaidi ya Wapalestina 2,300 katika Ukanda wa Ghaza kwenye mashambulizo ya kikatili ya siku 50 ya wanajeshi wa Israel ni sehemu ndogo tu ya jinai nyingi za kivita za utawala huo dhalimu. Ripoti ya Amnesty International dhidi ya Wapalestina imetolewa katika hali ambao hivi sasa Ukanda wa Ghaza unaishi katika hali nguvu sana kutokana na matatizo mengi kama vile uchache wa madawa, uhaba wa vifaa vya tiba, uchache wa mafuta na kukatika mara kwa mara umeme kutokana na vikwazo, kuzingirwa kila upande na mashambulizi ya mara kwa mara ya Wazayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo. Licha ya kuweko masaibu yote hayo, lakini shirika la msamaha la Amnesty International limethubutu kutoa ripoti na kudai eti Wapalestina wametenda jinai za kivita kwa kujibu jinai wanazotendewa kila leo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Radiamali ya HAMAS kuhusu ripoti ya Amnesty International

0 comments:
Post a Comment