TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

UN kupunguza kikosi chake cha kulinda amani DRC

UN kupunguza kikosi chake cha kulinda amani DRCUmoja wa Mataifa umetangaza kupunguza wanajeshi wake elfu mbili wa kwenye Kikosi cha Kulinda Amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO. Taarifa zinasema kuwa, Umoja wa Mataifa umeamua kupunguza wanajeshi wake elfu mbili wa kulinda amani nchini Kongo kati ya wanajeshi elfu ishirini walioko nchini humo. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesisitiza juu ya kuwepo mabadiliko, harakati na athari zaidi kwa kikosi hicho katika eneo la mashariki mwa Kongo. Uamuzi wa Umoja wa Mataifa unatolewa katika hali ambayo, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeutaka umoja huo kuwaondoa wanajeshi elfu sita wa kulinda amani nchini humo. Majeshi ya MONUSCO yamo nchini Kongo kwa muda wa miaka 15 sasa na yamejizatiti zaidi katika eneo la mashariki lililokumbwa na machafuko.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)