TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Inspekta wa Jeshi la Polisi auawa Mombasa, Kenya

Robert Kitur, Kamanda wa Polisi Kaunti ya MombasaInspekta wa Polisi Ibrahim Mohammed ameuawa kwa kufyatuliwa risasi na watu wenye silaha huko Mombasa, nchini Kenya. Jeshi la Polisi la Kenya limeeleza kuwa, watu hao waliobeba silaha hawakumjeruhi mtu yeyote baada ya kutekeleza shambulio hilo. Robert Kitur Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa amesema kuwa, bila shaka shambulio la kumuua Inspekta Ibrahim Mohammed lilipangwa na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, tokea serikali ya Kenya ilipoamua kupeleka majeshi yake nchini Somalia kwa shabaha ya kukabiliana na kundi la al Shabab, nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi na hasa katika Kaunti za Wajir, Mandera na Mombasa.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)