
Naibu mkufunzi katika timu ya
Manchester United Ryan Giggs amepinga madai ya mkwaruzano kati yake na
mkufunzi wa kilabu hiyo Louis Van Gaal.
Uvumi wa wasiwasi kati ya
makocha hao wawili ulizuka baada ya Giggs kukataa kusherehekea bao la
ushindi la Ashley Young siku ya jumatano.
Aliyekuwa mchezaji
mwenza katika kilabu hiyo Paul Scholes alisema kwamba Giggs amechoka
kuwa mkufunzi chini Ya Louis Van Gaal kwa miaka mitatu ijayo.
Lakini Giggs amesema kuwa wawili hao wana ushirikiano mzuri kati yao na kwamba anafurahia kazi yake chini ya mkufunzi Van Gaal.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment