TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Boko Haram watoto watu waliokuwa wakisoma Qur'ani

Boko Haram watoto watu waliokuwa wakisoma Qur'ani Magaidi wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wamewaua kwa umati wakaazi wa mji wa Gwoza waliokuwa wamekusanyika kusoma Qur'ani Tukufu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Wakaazi wa mji huo wamenukuliwa wakisema kuwa katika jinai hiyo ya Jumanne iliyopita, magaidi waliwaua kwa umati watu wasiopungua 68 wengi wao wakiwa vijana na watoto waliokuwa wamekusanyika katika kikao cha kusoma Qu'rani.  Mashuhuda wanasema Boko Haram walitumia silaha mpya kabisa katika kuzingira kikao hicho cha kusoma Qur'ani Tukufu na wakawafyatulia risasi kiholela waliokuwa hapo. Seneta wa eneo hilo Ali Nduwe amenukuliwa akisema kuwa magaidi wa Boko Haram waliuvamia mji huo wa Gwoza siku chache zilizopita na kuwaua wanaume huku wanawake na watoto wakilazimika kuyakimbia makazi yao.
Huku hayo yakijiri kinara wa Boko Haram ametangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL). Abubakr Shekau ametangaza kupitia mtandao wa kijamii wa twitter kuwa anamtii kiongozi wa kundi la kitakfiri la Daesh, Abubakr Baghdad. Katika siku za hivi karibuni magaidi wa Boko Haram wamekuwa wakitekeza jinai na ukatili sawa na ule wa kundi la Daesh kama vile kuwachinja na kuwateketeza moto watu wasio na hatia.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)