TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Ufisadi mabilioni wagunduliwa tena Ujenzi Tanzania

Ufisadi mabilioni wagunduliwa tena Ujenzi Tanzania Ikiwa machungu ya Watanzania bado hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya Wizara ya Ujenzi ya Tanzania. Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya (CAG) katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.
Kutokana na ufisadi huo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa Wizara ya Ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi kwa jamii na wahisani kuhusu bajeti.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)