TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

John Kerry kukutana na Rais Uhuru Kenyatta

NAIROBI, KENYA, WAZIRI wa maswala ya kigeni wa Marekani, John Kerry anatarajiwa kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kujadili masuala kadhaa yenye umuhimu wa kitaifa likiwamo suala la usalama na jinsi ya kulikabili kundi gaidi la Al Shabaab.
Kerry ambaye aliwasili nchini Jumapili alasiri, vilevile ameratibiwa kukutana na Kinara wa CORD Raila Odinga na viongozi wengine wa upinzani jijini Nairobi baadae Jumatatu.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Amina Mohammed amesema ziara ya Kerry ni ishara tosha kwamba uhusiano wa Kenya na Marekani ni imara.
Aidha, Waziri huyo anatarajiwa kuwahutubia wanahabari mwendo wa saa kumi na moja. Miongoni mwa masuala anayotarajiwa kuangazia ni, ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama mwezi Julai, msimamo wa Marekani kuhusu kundi gaidi la Al Shabaab na uhusiano wa mataifa haya mawili.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)