Umoja wa Mataifa umetangaza kupunguza
wanajeshi wake elfu mbili wa kwenye Kikosi cha Kulinda Amani huko
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO. Taarifa zinasema kuwa, Umoja
wa Mataifa umeamua kupunguza wanajeshi wake elfu mbili wa kulinda amani
nchini Kongo kati ya wanajeshi elfu ishirini walioko nchini humo.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesisitiza juu ya kuwepo mabadiliko,
harakati na athari zaidi kwa kikosi hicho katika eneo la mashariki mwa
Kongo. Uamuzi wa Umoja wa Mataifa unatolewa katika hali ambayo, serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeutaka umoja huo kuwaondoa
wanajeshi elfu sita wa kulinda amani nchini humo. Majeshi ya MONUSCO
yamo nchini Kongo kwa muda wa miaka 15 sasa na yamejizatiti zaidi katika
eneo la mashariki lililokumbwa na machafuko.UN kupunguza kikosi chake cha kulinda amani DRC
Umoja wa Mataifa umetangaza kupunguza
wanajeshi wake elfu mbili wa kwenye Kikosi cha Kulinda Amani huko
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO. Taarifa zinasema kuwa, Umoja
wa Mataifa umeamua kupunguza wanajeshi wake elfu mbili wa kulinda amani
nchini Kongo kati ya wanajeshi elfu ishirini walioko nchini humo.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesisitiza juu ya kuwepo mabadiliko,
harakati na athari zaidi kwa kikosi hicho katika eneo la mashariki mwa
Kongo. Uamuzi wa Umoja wa Mataifa unatolewa katika hali ambayo, serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeutaka umoja huo kuwaondoa
wanajeshi elfu sita wa kulinda amani nchini humo. Majeshi ya MONUSCO
yamo nchini Kongo kwa muda wa miaka 15 sasa na yamejizatiti zaidi katika
eneo la mashariki lililokumbwa na machafuko.

0 comments:
Post a Comment