Mohammed Abdul-Salam msemaji wa harakati ya al Houthi ya nchini Yemen amesema kuwa watu wa nchi hiyo hawataachana na mapinduzi yao kwa kuogopa vitisho.
Ameyasema hayo leo ikiwa ni siku moja baada ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kuliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kijeshi huko Yemen.
Siku kadhaa zilizopita nchi zisizopungua tisa zimefunga balozi zake na kuwaondoa wanadiplomasia wake huko Yemen kwa madai ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
0 comments:
Post a Comment