Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amekosoa vikali uingiliaji kati
wa kimataifa katika masuala ya nchi hiyo. Rais Joseph Kabila amepinga
vikali pendekezo la uungaji mkono wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa dhidi
ya waasi wa Kihutu wa FDLR wa nchini Rwanda walioko mashariki mwa nchi
hiyo. Matamshi ya Rais Kabila yanatolewa katika hali ambayo, siku chache
zilizopita, Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO
kilitangaza kusitisha utekelezaji wa operesheni ya pamoja na jeshi la
Kongo kwa lengo la kuliangamiza kundi la waasi wa FDLR, baada ya umoja
huo kuwatuhumu majenerali wawili wa jeshi la Kongo kwa vitendo vya
ukiukaji wa haki za binadamu. Rais Kabila amewaeleza wanadiplomasia
walioko mjini Kinshasa kwamba, jeshi la Kongo limeshaanza kutekeleza
operesheni ya kijeshi dhidi ya waasi wa FDLR huko mashariki mwa Kongo
bila ya msaada wowote wa vikosi vya MONUSCO. Umoja wa Mataifa umeeleza
kuwa, kuna waasi wa Kihutu wapatao 1,400 katika eneo la Ukanda wa
Maziwa Makuu ya Afrika kwa muda wa miaka ishirini sasa.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment