Vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimeeleza
kuwa , Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewahadaa wananchi baada ya kukurupuka
na kutangaza tarehe ya uchaguzi wa rais nchini humo. Taarifa
iliyotolewa na wapinzani nchini Kongo vimeeleza kuwa, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imetangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi wa rais bila ya
kuzingatia uhalisia wa mambo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, vyama vya
upinzani haviwezi kuipinga tarehe iliyoainishwa kufanyika uchaguzi huo,
bali imeeleza kwamba uamuzi huo wa tume umefanyika bila ya
kuwashirikisha viongozi, wanasiasa na wawakilishi kutoka makundi ya
kijamii na kiraia. Hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kongo
ilitangaza kwamba, uchaguzi wa rais nchini humo utafanyika tarehe 27
Novemba mwakani. Tume ya Uchaguzi ya Kongo ilitangaza kuwa uchaguzi wa
bunge nao utafanyika tarehe hiyohiyo. Hapo awali, serikali ya Kinshasa
ilifanya juhudi za kutaka kuakhirisha uchaguzi wa rais hadi mwaka 2018,
suala ambalo lililalamikiwa na kupingwa vikali na vyama vya upinzani na
makundi ya kiraia nchini humo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment