Timu ya Taifa ya Ivory coast imelamba dume.imeahidiwa kuzawadiwa mamilioni ya dola na Serikali ya nchi hiyo baada ya kutwaa kombe la mataifa Afrika.Rais Allassane Ouattara atawapatia wachezaji wote 23, kila mmoja Nyumba yenye thamani ya takriban dola elfu hamsini,na dola elfu hamsini nyingine mkononi.hii ni baada ya kuifunga Ghana kwenye Fainali za michuano hiyo.
Ghana nayo si haba haijaondoka mikono mitupu kwani Mdhamini wao Shirika la petroli la Taifa atampatia kila mchezaji wa dola elfu 25.
0 comments:
Post a Comment