
Meneja wa Southampton Ronald Koeman
ametoboa siri kuwa jana alilazimika kumwondoa Sadio Mane ambaye ni raia
wa Senegal kwenye orodha ya wachezaji watakaonza katika mechi dhidi ya
Liverpool kwa kosa la mchezaji huyo kuchelewa kuingia uwanjani.
Koeman
amesema ilibidi kumweka mchezaji huyo pembeni na kumpanga mchezaji
aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Benifica Philip Jurisichi kuchukua
nafasi yake.
Koeman alisisitiza kuwa timu hiyo imejiwekea kanuni ambazo ni lazima kila mtu azifuate .
Katika
mechi hiyo Southampton wakiwa nyumbani walipata kichapo cha magoli
mawili kwa bila majibu kutoka kwa Liverpool katika mechi ya lidi kuu ya
England.
Hata hivyo Koeman amejitetea kwamba pamoja na kipigo
hicho cha jana bado ana matumaini kuwa timu yake itamaliza msimu wa ligi
hiyo ikiwa katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment