TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

LEO KATIKA HISTORIA Jumanne, 17 Februari

Jumanne, 17 Februari, 2015
Leo ni Jumanne tarehe 27 Rabiuthani 1436 Hijria sawa na Februari 17, 2015.
Siku kama ya leo miaka 206 iliyopita, vilimalizika vita vya umwagaji damu vya Zaragoza vilivyopiganwa kati ya wanajeshi wa Ufaransa na wale wa Uhispania, huku Ufaransa ikipata ushindi na kuukalia kwa mabavu mji wa Zaragoza ulioko mashariki mwa Uhispania. Vita hivyo vilianza Novemba 15 mwaka 1808, kufuatia uvamizi wa jeshi la Napoleon.
Siku kama ya leo miaka 188 iliyopita, aliaga dunia Johann Heinrich Pestalozzi, msomi wa Uswisi na mmoja wa walimu mashuhuri. Pestalozzi alikuwa mjuzi wa elimu nyingi hasa hisabati na tiba na alizungumza lugha kadhaa za kimataifa. Msomi huyo wa Uswisi alikuwa na mtindo wake makhsusi wa kufundishia ambapo aliweza kutoa mafunzo ya masuala mbalimbali kwa watoto kwa wakati mmoja.
Na miaka 26 iliyopita katika siku kama leo, hati ya kuasisi muungano wa 'The Arab Maghreb Union' ilipasishwa nchini Morocco katika kikao kilichohudhuriwa na Marais wa nchi za kaskazini mwa Afrika. Muungano huo uliundwa kwa kuzishirikisha nchi za Libya, Algeria, Tunisia, Mauritania na Morocco. Muungano wa The Arab Maghreb Unioni ulianzishwa kwa shabaha ya kuunda taasisi moja ya kieneo ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi wanachama na hivyo kupunguza utegemezi kwa nchi za Magharibi. Hata hivyo hitilafu za kimitazamo zilizopo kati ya nchi wanachama wa muungano huo kama vile Algeria na Morocco kuhusu kadhia ya Sahara na vilevile baadhi ya hitilafu za kimipaka na kisiasa, yote hayo yamekwamisha kufikiwa malengo halisi ya muungano wa nchi za Kiarabu za kaskazini mwa Afrika.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)