uliokuwa makao makuu ya watawala wa Kiabbasi, ulitekwa na Hulagu Khan.
Hulagu alimuua mtawala al Muutasimu Billah na kukomesha kabisa
utawala wa kizazi cha Bani Abbasi uliotawala maeneo mengi ya ulimwengu
wa Kiislamu kwa kipindi cha miaka 37. Katika unyama huo mkubwa, Hulagu
Khan alifanya ukatili mkubwa na kuua nusu ya watu wasiokuwa na hatia wa
mji wa Baghdad. Hulagu Khan pia alichoma moto nyumba na majengo mengi ya
kihistoria ikiwemo maktaba kubwa ya Baghdad na idadi kubwa ya vitabu
vyenye thamani kubwa vya maktaba hiyo viliteketea au kutumbukizwa katika
mto Tigris.
Miaka 326 iliyopita katika siku kama ya leo tangazo lililojulikana kama Tangazo la Sheria lilisomwa katika sherehe za kumvika taji Mfalme William wa Tatu na Malkia Marry wa Pili wa Uingereza na kuanzia hapo mfumo wa utawala wa nchi hiyo ukabadilika na kuwa utawala wa kifalme wa kikatiba. Kwa mujibu wa tangazo hilo madaraka ya Mfalme wa Uingereza yalipunguzwa na kukabidhiwa Bunge la nchi hiyo.
Na tarehe 23 Rabiuthani miaka 191 iliyopita alifariki dunia faqihi, mwanachuoni wa hadithi na malenga mashuhuri wa Kiislamu, Allamah Ahmad Naraqi. Mwanazuoni huyo alizaliwa mwaka 1185 Hijria na kukulia katika mji wa Kashan katikati mwa Iran ambako alipata elimu kwa baba yake, Mullah Mahdi Naraqi. Miaka kadhaa baadaye alihamia katika mji mtakatifu wa Najaf, nchini Iraq na kupata elimu ya juu kwa maulamaa wakubwa wa mji huo. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu ameandika vitabu vingi vikiwemo vya “Miirajus Saada” na “Asrarur Hajj.”

0 comments:
Post a Comment