Muungano wa milki ya nchi za
kiarabu unasema kuwa unatuma ndege za kivita aina ya F-16 kwenda nchini
Jordan kusaidia taifa hilo katika harakati zake za kupambana na kundi la
Islamic State kama sehemu ya muungano unaongozwa na Marekani.
Jordan imeapa kuliangamiza kundi hilo ambalo lilimuua kinyama rubani wa ndege za kivita raia wake.Mashirika ya habari nchini humo yanasema kuwa hatua hiyo ni ishara ya uungwaji mkono unaopata Jordan kufuatia kujitolea kwake katika masuala ya usalama wa eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment